Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba na Mwenyekiti wa Sensa ya Watu na Makazi Mhe.Kanali Patrick Sawala ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kuhimiza waumini katika nyumba za Ibada kushiriki kuhesabiwa kwa ajili ya Maendeleo
Akizungumza na viongozi wa dini Agosti 10 2022 katika ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Dc Sawala amesema kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa ya kutoa elimu kwa waumini ili kuweza kupata takwimu sahihi
Ombi langu kwenu viongozi wangu wa Dini endeleeni kutoa elimu ya numuhimu wa sensa kwa waumini katika nyumba za Ibada ,sauti zenu ni sauti zenu ni sauti ya Mungu tunaamini sensa hii ifanyika kwa mafanikio makubwa kwa ushirikiano wenu,"amesema Dc Sawala
Aidha naye Mratibu wa Sensa Wilaya ya Tandahimba Ndugu Karim Mputa amesema kuwa Makarani wakatika maeneo husika Agosti 21 -22,2022 kwa ajili ya dodoso la Jamii ambalo litahoji huduma za Kijamii zilizopo katika eneo husika
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa