Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Kanali Patrick Sawala leo Agosti 4,2023 ametembelea Mabanda mbalimbali yakiwemo ya Halmashauri ya Mtwara, Vyama vya Ushirika, TRA, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na mabanda mengine kwenye Maonesho ya Nanenane, Kanda ya Kusini yanayofanyika kwenye viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Aidha, DC Sawala amevipongeza vikundi vya akina Mama na Vijana katika Mabanda hayo kwa kuonyesha namna wanavyojishughulisha ili kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza na Waandishi wa habari mara baada ya kutembelea maonesho hayo amewapongeza kwa maandalizi mazuri huku akiwasisitiza waoneshaji kuendelea kutoa elimu hata baada ya maonyesho hayo kuhusu fursa za kiuchumi na uwekezaji zilizopo katika Maeneo yao
"Hongereni vijana na vikundi vyote kwa kujiajiri Waelimisheni na vijana wengine waweze kuona fursa hizi..lakini pia Ukifanyakazi unapata heshima" DC Sawala
Kauli mbiu “ Vijana na Wanawake ni Msingi Imara wa Mifumo Endelevu ya Chakula”
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa