Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala amesema ameridhishwa na mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ya awali ya mfano shule ya msingi Mjimpya kata ya Tandahimba
Ameyasema hayo alipotembelea mradi huo unaotekelezwa na fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha Shilingi Mil.55 ambapo fedha hiyo inajenga vyumba viwili vya madarasa,ujenzi wa matundu ya vyoo sita na mfumo wa maji
“Nimeridhishwa na utekelezaji wa mradi huu,umekwenda kwa kasi nzuri lakini pia kwa ubora hivyo watoto wetu wa awali watasoma katika mazingira bora,”amesema Dc Sawala
Naye Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mjimpya Ndg.Shaibu Chinena amebainisha kuwa mradi upo hatua ya ukamilishaji ikiwa pamoja na kufunga michezo ya watoto
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa