Na. Kitengo cha Mawasiliano
Kuelekea Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru wa Tanzania Bara Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe. Kanali Patrick Sawala amewaongoza Watumishi na Wananchi kufanya Usafi wa Mazingira katika Hospitali ya Wilaya ya Tandahimba.
Akizungumza leo Disemba 8,2023 mara baada ya kukamilisha kufanya usafi,Dc Sawala amewapongeza wote walioshiriki kwenye zoezi hilo la usafi na kuwasistiza kuendelea kudumisha Amani na Umoja ambayo ni nguzo ya Maendeleo .
Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 62 ya Uhuru Wa Tanzania Bara ni Disemba 9,2023 ambapo Kiwilaya yataadhimishwa kwa bonanza la michezo mbalimbali na kisha kukamilisha kwa kufanya Mdahalo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ambapo pia Mgeni rasmi atakabidhi zawadi mbalimbali kwa wanafunzi washindi wa uandishi wa Insha.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa