Na Kitengo cha Mawasiliano
Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Kanali Patrick Sawala leo Agosti 23,2022 ameongoza wananchi wa Tandahimba kuhesabiwa katika Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi
Akizungumza mara baada ya Kuhesabiwa kwenye makazi yake kitongoji cha Mdenga Agosti 23,2022 Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba amesema zoezi linaendelea kwa amani na utulivu hakuna changamoto kubwa ambayo imejitokeza na wananchi wanaendelea kutoa ushirikiano kwa makarani
“Mimi tayari nimehesabiwa leo natoa wito kwa wananchi wa Tandahimba kuhesabiwa ili kupata takwimu sahihi kwa ajili ya Mipango wa Maendeleo ya Wilaya yetu na Taifa,”amesema Dc Sawala
Naye Mkurugenzi Mtendaji Halmsahauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndugu.Mussa Gama akizungumza mara baada ya kuhesabiwa kwenye makazi yake Kitongoji cha barabara ya tatu Kata ya Tandahimba Agosti 23,2022 amesistiza wananchi ambao bado hawajahesabiwa kuhakikisha wanaacha taarifa sahihi katika makazi yao
Mbunge wa Jimbo la Tandahimba Mhe.Katani Katani mara baada ya kuhesabiwa ametoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa makarani kwakuwa zoezi hilo linaendelea kwa siku saba hivyo litakamilika Agosti 29,2022
“Kama Karani hajafika leo basi atafika kesho zoezi hili linaendelea kwa siku saba hivyo toa ushirikiano kwa karani ili aweze kupata taarifa sahihi,”amesema Mhe.Katani
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa