Na Kitengo cha Mawasiliano
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Mhe.Mariam Chaurembo amesistiza ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo itawanufaisha wananchi
Amesema hayo katika kikao maalumu cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya(DCC) ambacho kimepitia mapendekezo ya Rasimu ya mpango .na Bajeti ya Wilaya kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba
Mhe Chaurembo amesema kuwa ili kuongeza ukusanyaji wa mapato usimamizi wa karibu unahitajika katika ukusanyaji wa mapato wa vituo vya afya sambamba na kufuatilia POS zote
‘ Tusitegemee zao moja la korosho angalieni na vyanzo vingine ambavyo vikisimamiwa vitaongeza mapato ya Halmashauri,lakini niwashauri ofisi ya TRA Wilaya kushirikiana pamoja na Halmashauri ili muweze kukusanya kodi,usipokusanya mapato ni ngumu kufikia malengo,”amesema Mhe.Chaurembo
Aidha Naye Mwenyekiti wa Halmsahuri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amepongeza ushauri uliotolewa katika kikao hicho na kuahidi kusimamia maelekezo na maazimio ambayo yametolewa katika kikao hicho
Katika kikao cha DCC Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imewasilisha rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo imekasimia kukusanya,kupokea na kutumia shilingi 41,581,076,000,TARURA Tandahimba imewasilisha mpango wa rasimu ya bajeti 2023/2024 shilingi 7.983,890,000,rasimu ya bajeti ya TFS Tandahimba shilingi 184,828,400, rasimu ya bajeti ya TRA Tandahimba shilingi 1,026,635,828 na RUWASA
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa