Na Kitengo cha Mawasiliano
Bodi ya Mfuko wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imefanya ziara na kukagua Miradi ya Elimu yenye thamani ya Tsh.Milioni 261.5 inayotekelezwa kwa Fedha za Mfuko wa Elimu sambamba na kukagua Maendeleo ya Kitaaluma kwa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari
Akizungumza wakati wa Ukaguzi huo leo Septemba 7,2023 Mwenyekiti wa Bodi hiyo Ndg.Msham Bakiri amewasisitiza Walimu kuzingatia taaluma na miiko ya kazi wawapo Shuleni ili kukuza taaluma kwa Wanafunzi akiwataka kuwaelemisha wazazi juu ya Umuhimu wa kuwapeleka watoto Shule
" Nitumie fursa hii kuwaasa Walimu kutimiza wajibu wenu na kuzingatia maadili ya kazi hii, walindeni watoto hawa, lakini pia jengeni mahusiano mazuri na wazazi ili iwe rahisi kwao kuwajibika kuwahudumia watoto wao mahitaji muhimu yanayohitajika," amesema Mwenyekiti wa Bodi
Kwa Upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mchichira Yusuph Msuya ameshukuru Mfuko wa Elimu Tandahimba kwa kuendelea kuboresha Elimu Shuleni hapo kwa kujenga Miundombinu ya Madarasa ambayo yamesaidia kuondoa upungufu madarasa uliokuwepo hapo awali na kuongeza ufaulu kwa Wanafunzi
Bodi ya Mfuko wa Elimu imekagua vyumba vya madarasa pamoja na matundu ya Vyoo katika Shule za Msingi Ruvuma, Mchichira, Namkomolela, Shule ya Sekondari Dinduma pamoja na ukamilishaji wa Bweni Shule ya Sekondari Kitama
Aidha fedha za Mfuko wa Elimu Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba hutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika sekta ya Elimu.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa