Na Kitengo cha Mawasiliano
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Sosthenes Luhende amefungua mafunzo ya usajili wa Mikorosho kwa Maafisa Kilimo, Watendaji wa vijiji na Makarani yanayotolewa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT).
Mafunzo hayo yanatarajiwa kuwasaidia maafisa hao katika kuendesha zoezo la usajili na kujua idadi ya wakulima na mashamba ya Korosho ili Serikali inapotoa pembejeo iweze kukidhi mahitaji ya wakulima.
Aidha, Luhende ameipongeza Bodi ya Korosho Tanzania kwa kuona umuhimu wa kutoa mafunzo kwa Maafisa hao.
"Mafunzo haya yakawasaidie kukasanya takwimu vizuri baada ya mafunzo haya tukafanye kazi kwa uadilifu,Kawasaidieni wakulima kutoa Takwimu sahihi za mashamba yao ili waweze kupata pembejeo stahiki zinazotolewa na Serikali "Luhende.
Mafunzo hayo yanatolewa kwa Maafisa Kilimo wa Kata na Vijiji ,watendaji vijiji pamoja na makarani.
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa