Na Kitengo cha Mawasiliano
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba limeridhia kupitisha rasimu ya Mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ambao umekasimia kukusanya na kupokea shilingi Bilioni arobaini na moja milioni mia tano themanini na moja na elfu sabini na sita elfu(41,581,076,000) kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo vyanzo vya mapato ya ndani
Akiwasilisha mapendekezo hayo ya mpango wa bajeti Februari 6,2023 kwa waheshimiwa madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Ndg.Mussa Gama amesema kuwa katika vyanzo vya mapato ya ndani Halmashauri imejiwekea lengo la kukusanya shilingi Bilioni tano milioni miatano hamsini na nane laki saba ishirini na saba elfu na mia tisa (5,558,727,900) kwa mwaka wa fedha 2023/2024
Aidha amesema ruzuku kutoka Serikali Kuu Halmashauri kwa mwaka 2023/2024 inatarajia kupata shilingi 24,804,449,00 kwa ajili ya mishahara,shilingi 3,459,664,000 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo , shilingi 940,636,000 kwa ajili ya matumizi mengineyo ,Fedha kutoka kwa wafadhili shilingi 6,817,599,000 na mapato yanayotokana na michango ya Jamii Halmashauri inatarajia kukusanya shilingi 850,000,000
Kwa upande wa matumizi ya fedha za mapato ya ndani Halmshauri imekasimia kutumia shilingi 5,400,000 kwa ajili ya Mishahara,shilingi 1.301,824,040 Miradi ya Maendeleo na matumizi mengineyo shilingi 1,963,764,960`
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa