Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba imepongezwa kwa kupata hati safi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali kwa miaka mitano mfullizo ikiwa ni miongoni mwa Halmashauri 17 zilizopata hati safi kwa miaka mitano mfululizo kati ya Halmashauri 185 nchini
Ndg Fasteki Mwampashe kutoka Ofisi ya CAG Mkoa wa Mtwara akisoma taarifa kwenyekikao maalum cha Baraza la madiwani
Akizungumza kwenye Kikao maalum cha Baraza la madiwani jana tarehe 15/06/2021 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Tandahimba mgeni rasmi ,Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Sebastian Waryuba ameipongeza Halmashauri kwa jitihada za kusimamia shughuli mbalimbali na kuwezesha Halmashauri kupata hati safi
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe.Sebastian Waryuba akizungumza jambo kwenye kikao maalum cha Baraza la madiwani
“Ni faraja kwa Mkuu wa Mkoa kuona Halmashauri zake zinapata hati safi,tunaipongeza sana Halmashauri kwa kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo, hati chafu ni mbaya hakuna anayeifurahia ,lakini pia tuendelee kusimamia bajeti ili malengo yaweze kufikiwa sambamba na kusimamia miradi ya maendeleo katika maeneo husika,”amesema Waryuba
Wakuu wa Idara na kamati ya ulinzi na usalama wakifatilia kwa makini kikao maalum cha baraza la madiwani
Aidha naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Said Msomoka akisoma taarifa ya jumla ya mwaka 2019/2020 ya ukaguzi wa hesabu za Halmashauri amesema katika mapendekezo 23 ambayo yamefanyiwa kazi ni mapendekezo 13 ambazo hoja zake zimefungwa na mapendekezo 10 hoja hazijafungwa lakini zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji
Mkurugenzi Mtendaji Ndg Said Msomoka akisoma taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2019/2020
“Katika mapendekezo hayo ambayo hayajafungwa taarifa ya miradi ya mfuko wa afya ina mapendekezo 4,mapendekezo 2 yamefanyiwa kazi na hoja zake kufungwa hivyo kubaki mapendekezo mawili na hoja zingine zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,”amesema Ndg Msomoka
Mwekahazina Ndg Ally Machela akielezea hoja ambazo zipo katika hatua za utrkelezaji
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa