Ujumbe kutoka Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Mkoa wa Songwe ukiambatana na Wakuu wa Wilaya na Wataalamu umefika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Kwa ziara ya Siku Mbili kwa ajili ya kujifunza jinsi Mfuko wa Elimu unavyotekeleza Miradi ya Maendeleo katika Wilaya hiyo.
Awali akitoa wasilisho la Bodi ya Mfuko wa Elimu mbele ya wageni hao Katibu wa Bodi ya Mfuko wa Elimu Tandahimba Christian Mazuge amesema katika kipindi cha Miaka 9 tangu kuanzishwa kwa Mfuko wa Elimu Mwaka wa Fedha 2015/2016-2023/2024 Jumla ya Tsh. Bilioni 7.2 imeweza kuboresha miundombinu ya Sekta ya Elimu katika
Wilaya hiyo.
Ametaja baadhi ya Miradi iliyotekelezwa na Mfuko wa Elimu ikiwemo Vyumba vya Madarasa 199 vimejengwa katika Shule za Msingi na Sekondari, Ujenzi wa Matundu 365 ya Vyoo, Ununuzi wa Madawati 13, 700, Ujenzi wa Vyumba 77 vya Maabara, Ujenzi wa Mabweni na Ujenzi wa Nyumba 36 za walimu.
Kadhalika Mfuko wa Elimu unaendelea na Ujenzi wa Shule Mpya ya Msingi Kijiji Cha Malamba yenye Gharama ya Tsh.Milioni 100 yenye Vyumba vinne na Ofisi.
ALAT Songwe imepongeza juhudi za Halmashauri ya Tandahimba Kwa kuboresha Elimu kwa Wananchi na kujenga miundombinu kupitia Mfuko wa Elimu na kuahidi kwenda kujifunza zaidi ili waweze kutekeleza katika Mkoa wa Songwe .
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba Mhe.Baisa Baisa amesema Wananchi wa Tandahimba wamekuwa na Mwitikio mkubwa wa kuunga juhudi za Serikali katika kuboresha Maendeleo ikiwemo Sekta ya Elimu na hivyo wamekuwa tayari kuchangia fedha kupitia Mfuko wa Elimu Kwa ajili ya Ujenzi wa Madarasa, Maabara, Vyoo sambamba na kununua Madawati.
#kaziiendelee
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa