Pichani: Wakimbiza Mwenge Kitaifa 2019 wakikagua mradi wa Maji Makonde
Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano
Miradi ya Maendeleo ya Wilaya ya Tandahimba yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 1.7 imeridhiwa baada ya kutimiza viwango na ubora vinavyotakiwa na Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mzee Mkongea Ally .
Alisema Katika Miradi hiyo ambayo ameizindua yote imekidhi vigezo na ubora unaotakiwa kama katika miradi ya madarasa lidumbe mtoni,chanzo cha maji mahuta na mradi wa maji Makonde
“Mwenge haupo kwa ajili ya kumuonea mtu wala kumpendelea mtu miradi hii tunayoizindua imekidhi ubora na vigezo vinavyotakiwa hivyo sisi tumeridhia,na tunawapa hongera kwa kazi nzuri ya kumuunga mheshimiwa Rais kwa kufanya katika uadilifu” alisema Mkongea Ally
Naye Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba katika taarifa yake kwa Mkimbiza Mwenge wa Uhuru alisema kuwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi katika Wilaya ya Tandahimba yamepungua
“Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika Wilaya yetu yanaonekana kupungua hii ni hatua nzuri lakini niwaombe wananchi waendelee kuchukua tahadhari kuhusu ugonjwa huu”, alisema Waryuba
TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA
Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA
Simu: +25523 2410030
Simu:
Barua pepe: ded@tandahimba.go.tz
Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa