• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

Halmashauri ya Tandahimba yatumia shilingi Milioni 145 kutengeneza samani za kidato cha kwanza

Posted on: January 7th, 2021

Na Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 145 zimetumika kutengeneza meza 2492 na viti 2552 kwa ajili ya maandalizi ya wanafunzi 3653 ambao wamechaguliwa kujiunga  kidato cha kwanza  Januari 11 mwaka huu katika Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

Akizungumza wakati wa kutembelea zoezi la kutengeneza samani hizo katika viwanda vidogo vidogo Mkuu wa Wilaya ya Tandahimba Sebastian Waryuba amesema kuwa  ameridhishwa na kasi ya utengenezaji wa samani hizo

Dc Waryuba (kulia) akimsikiliza Fundi (kushoto) akitoa maelezo kati ni Mkurugenzi Mtendaji Said Msomoka

“Nimetembelea ili niweze kuangalia kasi yao itatusaidia wanafunzi wetu kuvitumia viti na meza kwa wakati unaotakiwa,lakini kwakweli maendeleo ni mazuri naamini hadi kufika tarehe ya kufunguliwa shule tutakuwa tumefanikiwa katika zoezi hili naipongeza sana Halmashauri naMkurugenzi  kwa jitihada wanazozifanya,”amesema Dc Waryuba

Aidha Dc aliwashauri vijana ambao wanatengeneza vifaa hivyo kutumia vifaa maalum ili kuweza kuepuka madhara mbali mbali yanayoweza kuwapata kutokana na mionzi mikali inayotokana na kuchomelea

Dc Waryuba akitoa ufafanuzi wa jambo

Naye Mkurugenzi Mtendaji  wa Halmashauri ya Tandahimba Said Msomoka ambaye alikuwa kwenye ziara hiyo  amesema kuwa fedha hizo zimetolewa na mfuko wa elimu ili kufanikisha kupatikana kwa samani hizo kwa wakati muafaka

“Fedha hizi wametoa mfuko wa Elimu baada ya kutambua umuhimu wa jambo hili la  maandalizi ya kidato cha kwanza,  katika Halmashauri yetu tuna upungufu wa viti na mezakwa kidato cha kwanza  baada ya kutembelea kwenye shule zetu za sekondari 28 zilizopo na kukuta upungufu  huo,”amesema Mkurugenzi

 

Mkurugenzi Mtendaji ndg Msomoka (kati)akimweleza jambo Fundi (kushoto)

Kwa upande wa madarasa Mkurugenzi amesema kuwa Halmashauri kwa mwaka 2019/2020 iliweza kujenga vyumba vya madarasa zaidi ya 70 hivyo upungufu wa madarasa kwa kidato cha kwanza mwaka huu hakuna

    


Matangazo

  • Ratiba ya Usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi. January 03, 2018
  • Siku ya mazoezi kila jumamosi ya pili ya mwezi January 03, 2018
  • TANGAZO LA UJIO WA MWENGE WA UHURU 2018 WILAYANI TANDAHIMBA June 09, 2018
  • Soma

Habari mpya

  • TEA yakabidhi miradi kwa Halmashauri ya Tandahimba

    January 19, 2021
  • Halmashauri ya Tandahimba yatumia shilingi Milioni 145 kutengeneza samani za kidato cha kwanza

    January 07, 2021
  • Dc Waryuba awataka maafisa ugani wa vijiji na kata kuwa na mashamba ya mfano

    January 06, 2021
  • Mradi wa ufugaji kuku watua Tandahimba

    January 05, 2021
  • Soma

Video

Byakanwa Afunga mwaka kwa mikakati ya mabadiliko
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimba.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa