• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Ofisi |
Tandahimba District Council
Tandahimba District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Idara na Vitengo
    • Muundo wa Taasisi
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa Madiwani
    • Kamati
      • Kamati ya Fedha
      • Kamati ya Elimu, Afya na Maji
      • Kamati ya Uchumi, Ujenzi na Mazingira
      • Kamati ya Kudhibiti Ukimwi
    • Ratiba ya Vikao
    • Kumuona Mh. Mwenyekiti
      • Ratiba ya Kuonana na Mh. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyoko kwenye Mpango
    • Miradi Iliyoidhinishwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Zabuni
    • Kanuni na Taratifbu
    • Ripoti
    • Fomu za maombi
  • Kituo cha habari
    • Habari Mpya
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Hotuba
    • Video
    • Maktaba ya picha

Kamati ya CCM Mkoa wa Mtwara waridhishwa na Utekelezaji wa miradi ya maendeleo

Posted on: February 4th, 2020

Pichani: Kamati ya Siasa Mkoa wa Mtwara ikiwa kwenye picha ya pamoja na Kamati ya CCM Wilaya ya Tandahimba

Na Afisa Habari

Kamati ya Siasa Mkoa wa Mtwara imefanya ziara kukagua miradi ya maendeleo leo wilayani Tandahimba na kuridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo“Tumeiona,tumeridhishwa,kazi nzuri,inatia moyo”,Alhaj Saidi Kusilawe, Katibu wa CCM Mkoa wa Mtwara alisema.

Akizungumza wakati wa majumuisho baada ya ziara hiyo, Katibu huyo alisema kuwa Chama cha mapinduzi kimeamua kufanya ziara na kukagua miradi ya maendeleo kikiwa kinaelekea kilele cha maadhimisho kumbukizi ya miaka 43 tangu kuanzishwa ambapo kimkoa siku hiyo itaadhimishwa wilaya ya Mtwara vijijini katika Tarafa ya Nanyamba, Jimbo la Nanyamba tarehe 08.02.2020, “Ni Imani yangu nyote tutajumuika na karbuni tukienzi Chama cha Mapinduzi”, Kusilawe alisema.

Alhaj Kusilawe amewapongeza watendaji wilaya ya Tandahimba kwa kusimamia na kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi hususan ujenzi wa miradi ya maendeleo licha ya changamoto zinazoikabili wilaya hiyo; ametoa rai kwa watendaji kushirikiana na kushikamana kati ya chama na serikali ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Kamati ya Siasa CCM mkoa ilibaini changamoto ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayosimamiwa na TARURA ya mfumo  unaotumika kuwapata Wakandarasi ambapo huratibiwa na kusimamiwa na ngazi ya mkoa na kuwataka Mameneja wa wilaya kusimamia ujenzi wa miradi hiyo hali inayopelekea kukosa nguvu ya kuwawajibisha pindi wakandarasi wanapokiuka mkataba wa makubaliano.

Katika ziara hiyo Kamati ya siasa mkoa wa Mtwara ilifanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Lidumbe Mtoni na ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa katika shule ya msingi Nanhyanga.

Aidha Kamati hiyo ilikagua mradi wa umeme wa REA kijiji cha Nakayaka kata ya Chikongola pamoja na ujenzi wa Kalvati barabara ya Tandahimba – Mivanga na kumalizia jengo la Wadhibiti Ubora wa elimu wilaya.

Kamati ya siasa mkoa wa mtwara ikitoa maelekezo kwa Watendaji baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa shule ya msingi Lidumbe Mtoni

Kamati ya siasa mkoa wa mtwara ikijionea mradi wa Umeme wa REA kijiji cha Nakayaka kata ya Chikongola

Huo ni mradi wa ukamilishaji wa vyumba viwili vya madarasa shule ya msingi Nanhyangaambapo Kamati ya siasa mkoa wa mtwara ilipata fursa kujionea


Matangazo

  • TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI June 05, 2025
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI November 17, 2023
  • TANGAZO LA NAFASI YA KAZI YA MKATABA January 08, 2024
  • TANGAZO LA NAFASI YA MKIMBIZA MWENGE KIWILAYA March 30, 2024
  • Soma

Habari mpya

  • DC MNTENJELE AKAGUA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO SEKTA YA ELIMU

    June 25, 2025
  • DED MWANZALIMA ATEMBELEA MIRADI YA ELIMU

    June 21, 2025
  • TANDAHIMBA YAPATA HATI SAFI MARA YA TANO MFULULIZO.

    June 17, 2025
  • WAZIRI SIMBACHAWENE AMPONGEZA MKURUGENZI WA TANDAHIMBA NA MADIWANI KWA KUFANYA ZIARA YA MAFUNZO SIMIYU.

    June 11, 2025
  • Soma

Video

MKUU WA WILAYA YA TANDAHIMBA PAMOJA NA MKURUGENZI WASHIRIKI UJENZI WA KITUO CHA AFYA MAHEHA
Video nyingin

Kurasa za karibu

  • Ijue Tandahimba.

Viungio vinavyousiana

  • Ofisi ya Rais TAMISEMI
  • President's Official Website
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya sehemu

Tandahimba District Council

Wasiliana Nasi

    TANDAHIMBA DC,MTWARA TANZANIA

    Anuani ya posta: P.O.BOX 03 TANDAHIMBA

    Simu: +25523 2410030

    Simu:

    Barua pepe: ded@tandahimbadc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki ©2017 Tandahimba DC. Haki zote zimehifadhiwa